Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 50 2024-11-01

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatekeleza mkakati wa kujenga Zahanati kwenye Vijiji vyote nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Aidha, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2020/2021 hadi Septemba, 2024, Serikali imejenga na kukamilisha jumla ya zahanati 980 kote nchini.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa zahanati katika vijiji na mitaa umefanyika kimkakati kwa kuzingatia idadi ya watu na umbali kutoka kijiji na kijiji au mtaa na mtaa badala ya kila kijiji na kila mtaa kujenga zahanati. Hivyo, Serikali inaendelea kutenga fedha katika bajeti, kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za kimkakati katika maeneo yote nchini.