Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 125 2024-11-07

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:-

Je, lini Serikali itaboresha Kituo cha Afya Mtina ili kitoe huduma za upasuaji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya Mtina kilijengwa mwaka 1976 na ni moja ya vituo vya afya Kongwe 212 ambavyo Ofisi ya Rais, TAMISEMI imevibainisha kwa ajili ya ukarabati utakaoanza baada ya kukamilisha ukarabati wa hospitali kongwe za halmashauri. Hivyo Kituo cha Afya cha Mtina kitakarabatiwa wakati huo.