Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 429 2024-05-24

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza: -

Je, lini Serikali italipa fidia kwa wananchi waliopisha Mradi wa Umeme Kakono – Misenyi?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la tathmini ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa kilovoti 220 kutoka Kakono – Kyaka umekamilika na gharama za fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huu ni fedha za Kitanzania shillingi billioni 1.543. Malipo haya yanategemewa kuanza kulipwa hivi karibuni, ahsante.