Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 439 2024-05-27

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itahakikisha kunakuwa na maeneo maalum ya Watu wenye Ualbino kwenye mikutano ya hadhara ili wasikae juani?

Name

Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya 2004, kupitia matamko yake namba 3, Kifungu cha 11 - Uondoaji Vikwazo vya Ufikivu, 3:1-Matunzo kwa Watu wenye Ulemavu, 3(13) kuhusu Marekebisho na 3(14) - Mchangamano, imeonesha namna ambayo watu wenye ulemavu wakiwemo wenye Ualbino wanavyostahili kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za kijamii na kisiasa. Aidha, Sheria ya Watu wenye Ulemavu, Sura Na.183, Sehemu ya Nne, Kifungu cha 15(1) na Sehemu ya Tisa, Kifungu cha 51 zinabainisha juu ya ushiriki wa watu wenye ulemavu katika shughuli za kijamii na kisiasa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia nyaraka hizi muhimu, Serikali inatoa wito kwa viongozi wote wa Serikali na Taasisi zake pamoja na Taasisi na wadau wa huduma za kijamii kuhakikisha kuwa wakati wa utoaji wa huduma, suala la ufikivu na usalama kwa watu wenye Ualbino linazingatiwa. Aidha, Serikali inaendelea kutoa wito kwa watu wenye Ualbino kutambua mahitaji na haki zao kiafya na kujiepusha na mazingira yanayoweza kuhatarisha afya zao. Ahsante.