Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 49 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 632 | 2024-06-19 |
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa huduma ya maji bure vijijini kama ilivyo kwenye baadhi ya huduma za Elimu na Afya?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na.5 ya Mwaka 2019, Kifungu cha 43(1)(a), Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ina jukumu la kupanga, kusanifu na kujenga miradi ya maji vijijini. Aidha, baada ya miradi hiyo kukamilika, skimu za maji hukabidhiwa kwa Vyombo vya Utoaji wa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) ambavyo vimeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 32 na 33 cha sheria tajwa kwa ajili ya uendeshaji na matengenezo (Operation & Maintenance).
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia CBWSOs, jamii inahusishwa katika kupanga bei za utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi kwa kuzingatia teknolojia ya skimu inayotumika pamoja na hali ya uchumi ya jamii ya eneo husika. Vilevile, makundi maalum ya watumiaji wa maji katika jamii inayoweza kumudu gharama za uchangiaji na huduma hizo isiyoweza kumudu gharama za uchangiaji wa huduma hiyo kuwekewa utaratibu na kuyapatia huduma ya maji bure bila kuathiri shughuli za uendeshaji na matengenezo ya skimu.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved