Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 639 2024-06-19

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatafuta mwekezaji kwa ajili ya killimo cha miwa na Kiwanda cha Sukari katika Kata ya Mahenge Wilayani Kilolo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Bodi ya Sukari Tanzania imefanya upembuzi wa awali ili kubaini maeneo yanayofaa kwa kilimo cha miwa na uwekezaji wa viwanda vya sukari katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa. Matokeo ya upembuzi huo yameonesha kuna jumla ya hekta 11,746 zinafaa kwa uwekezaji huo zikiwemo hekta 8,945 katika Kata ya Nyazwa na hekta 2,801 katika Kata ya Mahenge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua zinazoendelea kutekelezwa ni upimaji wa maeneo hayo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo na baada ya hapo maeneo hayo yatakuwa tayari kwa ajili ya uwekezaji kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya nchi iliyopo kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania. Ahsante.