Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 10 2025-01-28

Name

Bahati Keneth Ndingo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbarali

Primary Question

MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya zoezi la Anwani za Makazi katika baadhi ya maeneo ya Rujewa, Imalilo, Songwe na Mwatenga ambayo bado hayajafanyika?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ulifanyika Februari hadi Mei 2022 kwa njia ya operesheni. Hatua hii ilikuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoyatoa tarehe 8 Februari, 2022. Kupitia Operesheni ya Anwani za Makazi Mfumo wa Anwani za Makazi ulitekelezwa nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ni endelevu kwa sababu ya mabadiliko ya makazi, wakazi na huduma. Ili kuweka mazingira endelevu ya utekelezaji kila mkoa na halmashauri ina mratibu/waratibu wa kusimamia utekelezaji, uendelezaji na matumizi ya mfumo.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI itatuma wataalam wake katika Halmashauri ya Mbarali kufanya ufuatiliaji, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo yaliyoainishwa na Mheshimiwa Mbunge ili kubaini mapungufu kwa ajili ya kuchukua hatua.