Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bahati Keneth Ndingo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbarali

Primary Question

MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya zoezi la Anwani za Makazi katika baadhi ya maeneo ya Rujewa, Imalilo, Songwe na Mwatenga ambayo bado hayajafanyika?

Supplementary Question 1

MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, na ninaipongeza Serikali kwa majibu mazuri. Ninaomba ufafanuzi kupitia maswali mawili.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; katika maelezo ya Serikali wamesema kwamba ilikuwa ni operesheni maalum kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais; lakini tunafahamu operesheni huwa inafanyika kwa kipindi maalum. Sasa twende na lipi, ni zoezi endelevu au ni operesheni?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kama ni zoezi endelevu, ni lini sasa maeneo yetu ya Mbarali ambayo yametoka hifadhini na kurudishwa kwa wananchi yatawekwa vibao vya anuani za makazi?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo. Kwanza, napokea pongezi na yeye pia ninampongeza sana kwa sababu anafuatilia sana mambo mengi yanayohusiana na masuala ya mawasiliano na teknolojia ya habari katika jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, suala hili lilianza kama operesheni maalum, lakini baada ya kufikia kiwango ambacho kiliridhisha, Mheshimiwa Rais aliporidhika, sisi kama Wizara tumefanya hii kuwa ni kazi endelevu kama ambavyo yeye ameuliza swali lake namba mbili.

Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya makazi yanaendelea kutokea mara kwa mara, majina ya makazi na vilevile teknolojia inavyoendelea kubadilika na biashara za mtandao zinavyoendelea kukua tunaendelea kuhitaji sana suala hili la anuani za makazi.

Mheshimiwa Spika, kwa swali namba mbili, niseme kwamba, maeneo haya ambayo yamerejeshwa tutatuma wataalam kwenda kwa Mheshimiwa Mbunge ili kulifanyia kazi na kuhakikisha nao pia wanapatiwa huduma hii.