Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2000-2005 Session 12 Sitting 6 Water and Irrigation Wizara ya Maji 97 2025-02-04

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: -

Je, lini miradi ya maji Wilayani Kyerwa itakamilika ili Wananchi wapate huduma ya maji?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia Theonest, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi sita ya maji katika Wilaya ya Kyerwa ambayo ni Runyinya - Chanya, Kikukuru, Kimuli – Rwanyango - Chakalisa, Kaisho - Isingiro, Nyamyaga - Nayakatera na Mabira. Hadi kufikia mwezi Januari, 2025, Serikali imekamilisha utekelezaji wa miradi miwili ya Nyamyaga – Nayakatera na Mibira ambayo inahudumia wananchi 26,218 waishio kwenye Kata za Bugomora na Mabira. Ujenzi wa miradi iliyobaki upo katika hatua za mwisho za utekelezaji na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2025.