Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, lini miradi ya maji Wilayani Kyerwa itakamilika ili Wananchi wapate huduma ya maji?

Supplementary Question 1

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, lakini kwa upekee sana nakuomba uniruhusu niseme haya. Hapa Bungeni Serikali imekuwa ikieleza mwaka 2024 wote kwamba inaenda kukamilisha mradi wa maji wa Kimuli – Rwanyango, mwaka mzima 2024 yamekuwa yakiongelewa haya lakini huo mradi haujakamilika na haujafanya chochote.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, siyo hilo tu, kuna miradi Serikali hapa inataja kwamba imekamilika, lakini hiyo miradi haitoi maji. Nayaongea haya kwa sababu Kyerwa ni moja ya Wilaya ambayo ina changamoto kubwa ya maji. Licha ya kukaa kwenye mabonde na kuwa na mito ya kutosha, lakini Kyerwa haina maji. Kwa hiyo, nayaongea haya kwa masikitiko.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ni lini hiyo miradi ya maji ambayo mmekuwa mkiitaja miaka yote itakamilika ili iweze kupunguza adha ya wananchi iliyopo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kukamilika kwa hiyo miradi itasababisha kuanza miradi mingine ili Kata kama za Rwabwere, Songambele, Bugara na Businde ambazo nimekuwa nikikutumia picha wakinywa maji machafu na waki-share maji na ng’ombe. Ni lini hizo kata zitaenda kupatiwa maji? Naongea kwa uchungu sana kwa sababu wananchi wa Kyerwa wanalalamika sana. (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, eneo la Kyerwa nimepata wasaa nami kuweza kufika, lakini kazi kubwa imefanyika na tuna miradi mingi ambayo inaendelea. Mheshimiwa Mbunge nakuomba, ukiangalia taarifa miradi mingi ipo kwenye 80%. Ukipata wasaa naomba leo tukutane, lakini kuna kazi ambayo ni kubwa inafanyika nami nilipata wasaa wa kwenda kuzindua baadhi ya miradi. Nataka niwahakikishie wana Kyerwa, moja ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania waishio mijini na vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwahakikishie Wanakyerwa jukumu hilo tunaliweza katika kuhakikisha miradi iliyobaki tunaikamilisha na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, ahsante sana.

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, lini miradi ya maji Wilayani Kyerwa itakamilika ili Wananchi wapate huduma ya maji?

Supplementary Question 2

MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kijiji cha Masimba ni miongoni mwa vijiji ambavyo bado vina changamoto kubwa sana ya maji Mvomero. Je, Mheshimiwa Waziri ni lini mtatupa shilingi milioni 950 ambazo tuliomba kwa ajili ya kumaliza tatizo hili la maji katika Kijiji cha Masimba? (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana na fedha. Tumeshaanza kupokea fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali. Nataka nimhakikishie kwamba maeneo ambayo ameyataja tutabana kuhakikisha tunapeleka fedha na wananchi hao wanapata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, lini miradi ya maji Wilayani Kyerwa itakamilika ili Wananchi wapate huduma ya maji?

Supplementary Question 3

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Mji wa Tukuyu, Wilayani Rungwe, una kata sita ambazo zinategemea tenki la maji, na Mheshimiwa Waziri, Aweso, alikuwepo wakati Mheshimiwa Rais anatoa maagizo kwamba lile tenki likamilike mara moja. Hata hivyo, mpaka sasa hivi tunaingia mwaka wa tatu lile tenki bado halijakamilika. Kata hizo sita za Bulyaga, Bagamoyo, Makandana, na Msasani mpaka sasa hivi, hakuna maji kwenye Kata zote za Ibigi kwa sababu tenki halijakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa busara na hekima za Mheshimiwa Waziri, naomba hawa watu wa Wilaya ya Rungwe wapate majibu sahihi juu ya tenki lao lile ambalo liko muda mrefu sana. (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, tulipata concern ya madai ya mkandarasi juu ya utekelezaji. Katika ule mradi pamoja na ujenzi wa tenki pia tulifanya pass way ili kuhakikisha watu wanapata huduma ya maji safi na salama. Hata hivyo, alikuwa anadai kiasi cha shilingi milioni 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuhakikishia kwamba tumeshamlipa na hawana kisingizio chochote. Kwa hiyo, jukumu lao ni kuhakikisha kazi ile inakamilika na wananchi wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama, ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, lini miradi ya maji Wilayani Kyerwa itakamilika ili Wananchi wapate huduma ya maji?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya maji ya Mwika Kaskazini na Mwika Kusini ambayo ilikuwa imetengewa shilingi bilioni 2.7 ndani ya bajeti ya miaka mitatu iliyopita, lakini haijapewa fedha hata kidogo na kazi ndogo iliyofanyika pale imetokana na fedha za ndani kutoka kwenye mamlaka husika. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kutoa tamko kwamba sasa fedha hiyo itaachiliwa ili miradi hiyo ikamilike na mwanamke wa Mwika Kaskazini na Kusini atuliwe ndoo? (Makofi)

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, namhakikishia Mzee wangu, Mheshimiwa Dkt. Kimei kwa kuwa kipindi hiki tupo katika kipindi cha Bunge apate wasaa wa kufika ofisini tuone namna ya haraka tunaweza kuwasaidia wananchi wa Mwika, ahsante sana.