Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Finance and Planning Wizara ya Fedha 106 2025-02-04

Name

Michael Mwita Kembaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza:-

Je, Serikali inachukua hatua gani kwa Wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya Kampuni kwa lengo la kukwepa kodi?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Mwita Kembaki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua changamoto ya ukwepaji wa kodi unaosababishwa na mabadiliko ya majina ya kampuni za kigeni, Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti mianya hiyo ya ukwepaji wa kodi. Hatua hizi ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Kampuni, Sura 212, ambayo inawataka wawekezaji kutoa taarifa kwa Msajili wa Kampuni (BRELA) wanapobadilisha jina la kampuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, historia ya mabadiliko yote ya majina huhifadhiwa kwenye kumbukumbu rasmi ili kuhakikisha kuwa majina mapya hayawezi kutumika kuficha madeni ya kodi au kushiriki katika shughuli zisizo halali. Aidha, kupitia Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura 438, Serikali imeweka sharti kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itahakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina. TIN hutumika kufuatilia historia yote ya ulipaji kodi wa kampuni, hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wala kufuta wajibu wa kodi.