Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 128 2025-02-06

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:-

Je, Wakuu wa Wilaya wametekeleza kwa kiasi gani agizo la Waziri Mkuu la kutenga ofisi za watu wenye ulemavu katika ofisi zao?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu aliyoyatoa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Watu Wenye Ulemavu, Mkoani Dar es Salaam Agosti, 2023, mikoa kwa kushirikiana na halmashauri imeendelea kuratibu upatikanaji wa Ofisi za Vyama vya Watu Wenye Ulemavu.

Mheshimiwa Spika, kufikia Januari, 2025 Mikoa 26 na Wilaya 73 zimetenga ofisi za Vyama vya Watu Wenye Ulemavu katika majengo ya Halmashauri, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Ofisi za Kata.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha ofisi za Vyama vya Watu Wenye Ulemavu zinapatikana katika wilaya zote nchini. Ahsante.