Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:- Je, Wakuu wa Wilaya wametekeleza kwa kiasi gani agizo la Waziri Mkuu la kutenga ofisi za watu wenye ulemavu katika ofisi zao?

Supplementary Question 1

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na naomba niipongeze Serikali kwa jitihada ambayo wameifanya kwa kuweza kufikisha 60% ya kutafuta Ofisi za watu wenye ulemavu. Ninaomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuweza kupata hizo ofisi na jitihada ambazo zimefanyika, nilikuwa nina ombi la kwamba tulete marekebisho ya sheria ili sasa hili lisiwe agizo peke yake la Mheshimiwa Waziri Mkuu basi iwe sheria rasmi ambayo haitoweza kuondolewa mpaka nafasi ya watu wengine itakapokuja. Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Khadija Taya mara kwa mara amekuwa akifuatilia maslahi na ustawi wa watu wenye ulemavu na Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapewa stahiki zao, lakini pia wanatengenezewa mazingira bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwanza, nimhakikishie kwamba maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatekelezeka, lakini pia wazo lake la kuwa na sheria au sera maalum kwa ajili ya hilo tumelipokea tutalifanyia kazi na kuona uwezekano wa kuendelea na utaratibu huo. (Makofi)