Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 41 2025-01-30

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaweka mkakati madhubuti wa upatikanaji wa maji ya uhakika kwenye Shule za Msingi na Sekondari nchini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa maji ya uhakika kwenye shule za msingi na sekondari nchini. Mikakati hiyo ni pamoja na kutoa fedha kwa baadhi ya shule kwa ajili ya kuchimba visima virefu na vifupi, kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kuvuna maji ya mvua na kununua matanki makubwa kwa ajili ya kuhifadhia maji na kutoa elimu ya namna ya kuhifadhi vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo yao ili maji hayo yasaidie kutumiwa na shule zilizopo jirani na vyanzo hivyo.
Mheshiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wizara ya Maji kuhakikisha kuwa shule za msingi na sekondari zinapata vyanzo vya maji vya uhakika.