Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 42 2025-01-30

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasikiliza Wananchi wa Kitongoji cha Bandabichi, Kijiji cha Ifunda, ambao walihamishiwa katika Kijiji cha Kivalali bila ridhaa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya mipaka ya maeneo ya utawala yamekuwa yakifanyika kwa kuzingatia Mwongozo wa Uanzishaji wa Maeneo ya Utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014. Serikali kupitia barua yenye Kumb. Na. CFA.89/141/01/"C"/19 ya tarehe 16 Januari, 2024 ilipokea ombi la kuhamishwa Vitongoji vya Kibaoni B, Bandabichi na Ifunda Sekondari vilivyopo Kijiji cha Bandabichi, Kata ya Ifunda, vihamie Kijiji cha Ifunda. Aidha, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeshafanyia kazi maombi hayo na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 796 la Agosti, 2024.

Mheshimiwa Spika, ikiwa kusudio la sasa ni kukirejesha Kitongoji cha Bandabichi katika Kijiji cha Bandabichi kilipokuwa awali, naishauri halmashauri kufuata utaratibu ulioainishwa kwenye Sheria ya Uanzishwaji wa Maeneo ya Kiutawala kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji.