Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasikiliza Wananchi wa Kitongoji cha Bandabichi, Kijiji cha Ifunda, ambao walihamishiwa katika Kijiji cha Kivalali bila ridhaa?

Supplementary Question 1

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, kwanza naishukuru Serikali kwa hizo hatua za awali na mchakato umeshaanza. Ombi langu, ni kwamba huo mchakato ukamilike kwa maana hata hilo eneo la Bandabichi tayari limeshaombewa. Ahsante sana kwa hatua hiyo, sina swali la nyongeza.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimepokea. Tutafuatilia kwa karibu ili waweze kukamilisha hizo hatua na sisi tutachukua hatua kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasikiliza Wananchi wa Kitongoji cha Bandabichi, Kijiji cha Ifunda, ambao walihamishiwa katika Kijiji cha Kivalali bila ridhaa?

Supplementary Question 2

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwenye Jimbo la Ndanda, Vijiji vya Pangani, Sululu ya leo na vijiji vingine vingi kwa muda mrefu vimeleta maombi kwenye Wizara hii ya TAMISEMI ili kuweza kupata namba za vijiji. Nataka kufahamu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, je, ni lini vitongoji hivyo vitapata namba za vijiji kwa sababu ni vikubwa sana na vinakidhi vigezo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Cecil Mwambe, tuweze kuwasiliana kufanya ufuatiliaji wa hatua ambayo maombi hayo yamefikia ili tuweze kuyafanyia kazi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI.