Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 43 2025-01-30

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: -

Je, kwa nini ajira za muda kama za kuandikisha wapiga kura zisitolewe kwa watu wasio na ajira badala ya kuwapa watu walioajiriwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ajira za muda za uandikishaji wa wapiga kura zipo kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (2) ya Kanuni za Uchaguzi za Mwaka 2024. Tangazo la Serikali Na. 572 na Kanuni ya 10 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2024, zinaelekeza Msimamizi wa Uchaguzi kufanya uteuzi wa watumishi wa umma watakaoandikisha na kuandaa orodha ya wapiga kura.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024, shughuli nyingine za ukarani (usaidizi katika vituo) zilitolewa pia, kwa watu wasio na ajira katika vituo vipatavyo 80,584.