Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, kwa nini ajira za muda kama za kuandikisha wapiga kura zisitolewe kwa watu wasio na ajira badala ya kuwapa watu walioajiriwa?

Supplementary Question 1

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, mara nyingi Serikali imekuwa haitoi fursa kwa wasomi ambao wamewasomesha wenyewe na hivyo, kujinyima haki ya kutumia fursa hizo, halikadhalika wamekuwa wakitoa ajira kwa watu ambao tayari wana ajira. Hawaoni kwa kufanya hivyo wanazorotesha huduma zinazotakiwa kutolewa na waajiriwa hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia, kwa kufanya hivyo, hawaoni kuwa, inawanyima fursa watu wasiokuwa na ajira angalau wapate kifuta machozi? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Issa Mchungahela kwamba, Serikali inatambua na inathamini vijana ambao wamehitimu na wanataaluma tofauti tofauti na ina dhamira ya dhati kabisa ya kuweza kuwaajiri katika hizi ajira rasmi. Serikali imekuwa ikifanya hivyo, ikitangaza ajira na vijana wamekuwa wakiomba nafasi hizo. Kwa hiyo, Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na wasomi na kuwatumia katika Serikali.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, kwa muktadha wa kazi hii katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuandaa orodha ya wapigakura, Sheria na Kanuni zimetoa mwongozo wa kutumia watumishi wa umma kwa ajili ya kufanya kazi hii, lakini kuna kada nyingine ambazo ajira zinatangazwa na Serikali na wasomi wetu wanaweza kuomba.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kuendelea kuwapa moyo Watanzania ambao wamesoma, wana vyeti vyao na wanatafuta ajira, wafuate utaratibu. Serikali inapotangaza ajira waweze kuomba na watapata ajira kwa nafasi zinazokuwa zimetangazwa.