Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 44 2025-01-30

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM aliuliza: -

Je, tathmini ipoje juu ya maendeleo ya kaya maskini zilizodhaminiwa na TASAF kwa upande wa Zanzibar?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, tathmini kubwa ya Kipindi cha Kwanza cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ilikamilika Mwaka 2019 na kipindi cha pili itakamilika mnamo Juni, 2025. Kwa upande wa Zanzibar, Tathmini kubwa ya kipindi cha kwanza cha Mpango ilionesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali kama vile, walengwa wanapata mahitaji ya msingi ya maisha kama vile chakula, vifaa vya skuli kwa watoto na makazi ya kuishi kuboreshwa; kuongezeka kwa mahudhurio ya watoto shuleni kufikia 95% na pia, viwango vya ufaulu; wazazi kupeleka watoto kliniki kwa zaidi ya 95%, kwa ajili ya ushauri wa kitaalam; na kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika shehia hivyo, kuchochea ukuaji wa shughuli za uchumi katika maeneo hayo.