Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 45 2025-01-30

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaunda Mamlaka ya Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ili kuimarisha usimamizi wa uwekezaji ndani ya Serikali?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, uundwaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma unasubiri kupitishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma, ambapo Muswada wa sheria hiyo, umesomwa kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2023 na kuelekezwa kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa ajili ya uchambuzi. Mara baada ya Kamati kukamilisha kazi hiyo, Muswada huo utaletwa hapa Bungeni kwa ajili ya hatua nyingine zinazofuata za utungwaji wa sheria.