Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: - Je, lini Serikali itaunda Mamlaka ya Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma ili kuimarisha usimamizi wa uwekezaji ndani ya Serikali?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Tunatambua kwamba kuna Watanzania ambao wanaishi nchi za nje kama diaspora. Sasa ni nini mkakati wa Serikali wa kuweka incentive kwa ajili ya kuwavutia Watanzania ili waje kuwekeza Tanzania?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, EPZA wamechukua eneo la zaidi ya ekari 3,000 kwa ajili ya uwekezaji. Sasa, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba lile eneo ambalo wamelitenga Manyoni linatumika kwa ajili ya uwekezaji? Ahsante sana.
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu, sasa tunakwenda kwenye marekebisho ya sheria kuweza kuwatambua diaspora kuwa na uraia maalum hapa nchini. Pia tunatambua kabisa kwamba uvutiaji wa wawekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji cha TIC tunawakaribisha hawa wawekezaji kutoka nje na tunawapa incentive pale wanapokuwa wanakuja na mtaji unaozidi zaidi ya Dola 200,000. Kwa Watanzania, tunawapa incentive pale wanapokuwa wamewekeza mtaji wa zaidi ya Dola 50,000.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa raia, hawa wa diaspora tutaangalia namna ya kuwavutia na wao wawe na punguzo kidogo ambalo litawafanya waweze kuvutiwa zaidi kuja kuwekeza hapa nchini Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, ni kweli EPZA imechukua maeneo ya Manyoni zaidi ya ekari 3,000 na imechukua maeneo haya maalum kwa ajili ya uwekezaji. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, mikakati bado inaendelea na wananchi wa maeneo hayo waliochukuliwa maeneo yao watalipwa na uwekezaji utaendelea katika eneo hilo, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved