Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2000-2005 Session 12 Sitting 3 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 46 2025-01-30

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, lini vijiji vya Bukene na Itobo vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama vijiji vingine?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali halisi ilivyo nchini, kuna maeneo ya vijiji na vijiji miji. Serikali inaendelea kuwahakikishia wananchi kwamba maeneo yote ya vijiji yataendelea kuunganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000. Maeneo ya Bukene na Itobo ni vijiji miji, hivyo, gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 320,960. Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho kutokana na tathmini iliyofanyika, ahsante.