Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, lini vijiji vya Bukene na Itobo vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama vijiji vingine?

Supplementary Question 1

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kama Kijiji cha Bukene ni kijiji mji, inakuwaje kwamba katika kijiji hicho hicho cha Bukene ambacho kina transfoma nne ukijiunganisha kwenye transfoma moja, unatozwa shilingi 27,000, lakini ukijiunganisha kwenye transfoma nyingine ni shilingi 320,000 wakati ni kijiji kimoja? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Itobo ambayo pia imesemwa ni kijiji mji ina vitongoji vinne au vitano, lakini kitongoji kingine kinatozwa shilingi 27,000 na kitongoji kingine kinatozwa shilingi 320,000/= wakati vitongoji vyote vinaunda kijiji kimoja. Kwa hiyo, hii inaleta mkanganyiko kwa wananchi. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Tayari nimemwelekeza Meneja wa Nzega na Meneja wa Mkoa wa Tabora wafike katika maeneo ya Bukene na Itobo, wafanye tathmini ili tuweze kupata majibu ya kina ili kuweza kuondoa mkanganyiko huo. Kwa hiyo, narudia tena kumwelekeza Meneja wa Wilaya ya Nzega na Tabora wafanye tathmini hiyo kwa Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kutatua suala hili ambalo limejitokeza, ahsante. (Makofi)

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, lini vijiji vya Bukene na Itobo vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama vijiji vingine?

Supplementary Question 2

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara bado ina maeneo ya vijiji kama vile Katindiuka, je, ni lini ombi letu kwa wananchi wa Katindiuka kuunganishiwa umeme kwa shilingi 27,000 litafanyiwa kazi? Ahsante.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, maeneo ambayo yanaunganishwa kwa shilingi 27,000 ni maeneo ya vijiji na shilingi 27,000 ni kutokana na nature ya miradi yenyewe ambayo Serikali inaweka fedha, na pia kuna fedha za wafadhili katika kutekeleza miradi hiyo. Kwa hiyo, siyo kila eneo linakidhi vigezo hivyo vya shilingi 27,000. Maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyasema hapa ya vijiji A na B yanapata tathmini ya mitaa. Kwa hiyo, tutaendelea kuangalia kwa kina kama yanakidhi vigezo vya shilingi 27,000 na kama hayakidhi, basi gharama yake ya kuunganisha ni shilingi 320,960/=, ahsante.

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, lini vijiji vya Bukene na Itobo vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama vijiji vingine?

Supplementary Question 3

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nataka kujua ni lini vijiji vilivyosalia Kyerwa vitapatiwa umeme ikiwepo Kijiji cha Bugaza ambacho kipo Kata ya Kimuli, na pia Kijiji cha Nyarugongo kilichopo Businde?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwa maeneo ya Kyerwa umeme umeshafika katika makao makuu ya vijiji. Tutaendelea kuangalia kama mkandarasi hajamaliza zile kilometa mbili za ziada. Kwa hiyo, nitafuatilia kwa vijiji hivi viwili, lakini kwa taarifa ambayo tunayo katika makao makuu ya Kijiji, umeme umeshafika. Ahsante.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, lini vijiji vya Bukene na Itobo vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama vijiji vingine?

Supplementary Question 4

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itakamilisha kwa haraka mradi wa ujazilizi katika Wilaya ya Karatu ambao unasuasua?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Mkandarasi wa mradi wa ujazilizi yupo site, tutamfuatilia na tutaendelea kumsimamia kwa weledi ili kuhakikisha anakamilisha mradi huo kulingana na muda ambao umewekwa, ahsante.