Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 8 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 133 | 2025-02-06 |
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mji Mdogo wa Karatu ni wastani wa 75%. Mahitaji ya maji katika Mji huo ni wastani wa lita 8,750,000 kwa siku wakati uzalishaji ukiwa ni wastani wa lita 5,919,000 kwa siku.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma ya maji inakuwa toshelevu kwenye Mji huo, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bwawani Na. 3 kwa ajili kunufaisha kata tatu za Karatu, Ganako na Qurus. Mradi huo umefikia wastani wa 77% za utekelezaji na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2025.
Mheshimiwa Spika, vilevile, katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali itatekeleza mradi wa kuongeza uzalishaji wa maji katika Mji huo kwa kuchimba kisima kimoja pamoja na kuendeleza visima viwili vilivyopo katika eneo la Qorong’aida.
Mheshimiwa Spika, aidha, kazi zingine zitakazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tanki la lita 50,000, ukarabati wa matanki manne yenye jumla ya ujazo wa lita 625,000 na ununuzi na ufungaji wa dira za maji 2,000. Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2025. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved