Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza, naishukuru na kuipongeza Serikali kwa majibu na kwa jitihada ambazo zinaendelea ili kuhakikisha kwamba upungufu wa maji unakwisha kabisa. Swali la kwanza, Je, Serikali sasa inawahakikishiaje wananchi kwamba, miradi hii ikikamilika upungufu huu wa maji katika Mji wa Karatu unakwisha kabisa? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali haioni ni wakati sasa wa kuipatia ruzuku miradi ya maji iliyoko pembezoni mwa Mji wa Karatu ambayo inaendeshwa na Bodi ya Wananchi ikiwemo Endawasu, Gewasu na Mowasu ili wananchi waweze kupata maji kwa uhakika? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, Serikali inatambua changamoto kubwa iliyopo, lakini mradi huu utakapokamilika siyo kwamba changamoto itaisha kwa 100%, isipokuwa huduma ya upatikanaji wa maji katika mji huo itaongezeka kutoka 75% mpaka kufikia 82%. Kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha kwamba tunasanifu miradi ambayo itaenda kupanua wigo wa upatikanaji wa maji mpaka kufikia katika hatua ambayo itaridhisha kwa wananchi wote kupata hiyo huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Spika, vile vile, katika kipengele cha pili, ninaendelea kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya nasi tunatambua Bodi za Maji za Gewasu, Endawasu pamoja na Mowasu ni bodi ambazo bado zinasimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Mheshimiwa Spika, maana yake ni kwamba, hata ujenzi wa miradi yenyewe inajengwa na RUWASA, pia tumeshapata mtaalam mshauri ili kwenda kuangalia namna bora ya kuendelea kupata vyanzo vingine vya maji ili tujenge mtandao ambao utakaowafikia wananchi wote ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali kupitia Wizara ya Maji tunaendelea kuifanya kazi hiyo vizuri sana. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Martha Nehemia Gwau
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 2
MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Spika, suala la upungufu wa maji bado linakabili Wilaya za Manyoni, Iramba na Singida Mjini. Ni lini mradi wa Miji 28 utakamilika ili kutatua changamoto hiyo iliyopo kwa sasa? Ninashukuru. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge, lakini na Waheshimiwa Wabunge wote ambao wanaendelea kuupambania Mradi huu wa Miji 28. Bahati nzuri wiki moja iliyopita nilikuwepo Manyoni kukagua utekelezaji wa mradi huo na namna ambavyo unaenda kukamilika. Ifikapo Oktoba mwaka huu mradi huu utakuwa umekamilika na wananchi watapata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
Name
Aysharose Ndogholi Mattembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 3
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. Ninapenda kufahamu ni lini sasa Serikali itakamilisha miradi yote ya maji katika Mkoa wa Singida? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwa maelekezo mahsusi ni kwamba, kuna miradi zaidi ya 1,000 inayoendelea kutekelezwa nchi nzima na kuna miradi ambayo inaendelea kutekelezwa ndani ya Mkoa wa Singida.
Mheshimiwa Spika, miradi hii iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwa kadri watakavyokuwa wanaomba pesa za kulipa kulingana na madai ya wakandarasi, basi miradi hiyo itaendelea kukamilika kulingana na mkataba ambao tutakuwa tumeingia na wakandarasi. Ahsante.
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 4
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali mna mkakati gani wa kumaliza mgao wa maji ndani ya Kata za Buza, Kilakala, Makangarawe na nyinginezo ndani ya Jimbo la Temeke? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Temeke na kwa Mkoa wa Dar es Salaam chanzo chake cha maji ni kutoka Mkoa wa Pwani. Tuko katika upanuzi wa vyanzo vya maji kwa kuanzisha miradi mbalimbali ili lengo tuwe na maji ya kutosha.
Mheshimiwa Spika, tukiwa na maji ya kutosha, maana yake ni kwamba tutakiwa na uwezo wa kuwafikishia wananchi wote maji kwa wakati wote bila kuwa na mgao. Kwa sasa ni lazima tukiri kwamba, mgao bado upo, lakini tunahakikisha mgao huu unakuwa predictable. Maana yake tukishasema Jumatatu au Jumatano, basi watu wa maeneo husika waweze kuwa na uhakika wa kupata maji katika siku hizo ambazo tumewapangia mgao huo.
Mheshimiwa Spika, juhudi za Serikali zinaendelea; tunaendelea kujenga mabwawa mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kwamba tunapata zao la maji la kutosha ili wananchi wa Kinondoni, Kibamba, Temeke na wa Kigamboni, wote wapate huduma ya maji safi na salama na yawe toshelevu na yenye gharama ambayo inakubalika. Ahsante sana.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 5
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Sirari, Nyamwaga na Nyamongo, umesimama kabisa na Tarime kwa ujumla wake kuna shida ya maji. Je, nini kauli ya Serikali ili mradi uweze kuendelea ili watu wa Tarime wapate maji? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, lakini hapa Katikati tulikuwa na changamoto, tunawashukuru sana Wizara ya Fedha na tunamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo ya kutoa fedha kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ili wakandarasi warudi site na waendelee na utekelezaji ili miradi hiyo ikamilike.
Mheshimiwa Spika, kati ya miradi ya kimkakati ni pamoja na mradi ambao Mheshimiwa Mbunge ameutaja. Ninakuhakikishia kuwa tutaendelea kuhakikisha kwamba, miradi yote ambayo inaenda kuleta mabadiliko na kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji, tutaisimamia kikamilifu ili iweze kukamilika kwa wakati. (Makofi)
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 6
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini maji kutoka Lake Victoria yatafika Urambo ili tumalize tatizo kubwa la maji tulilonalo? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mradi wa kufikisha maji kwenda Urambo unatokana na mradi mkubwa ulioanza wa shilingi bilioni 680, ambapo extension yake ni Urambo pamoja na Kaliua. Tayari shilingi bilioni 143 imetengwa kwa ajili ya mradi huo na sasa mabomba yameshafika site na mradi huu uko katika 65%. Tunatarajia muda siyo mrefu ninaamini kwamba kabla ya mradi wenyewe kukamilika kuna maeneo mengine yataanza kupata huduma ya maji wakati utekelezaji ukiwa unaendelea katika kukamilisha. Ahsante sana.
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 7
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Mradi wa Maji wa Kata ya Ng’ang’ange utaanza kufanya kazi kwa sababu toka mwaka jana ulikuwa umesainiwa na Serikali? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninaukumbuka mradi huu kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameuongelea, uko katika Jimbo la Kilolo. Bahati nzuri katika utiaji wa Saini nilikuwepo mimi mwenyewe, ilikuwa mwaka jana mwezi Mei. Mkataba huu ni wa miezi 12 ambao gharama yake ni zaidi ya shilingi milioni 987 na mkandarasi mpaka sasa ameshalipwa shilingi milioni 148 na kazi hii inatekelezwa na Mkandarasi anaitwa Afrocentric Company Limited.
Mheshimiwa Spika, tunaamini kabisa kwamba kwa kazi ambayo tayari ameshaianza, ameshajenga foundation ya tenki na ameshaleta mabomba, kwa hiyo tunaamini kwamba, kwa kasi anayoenda nayo tunaamini kwamba atakamilisha ndani ya muda wa mkataba ambao tulikubaliana naye. (Makofi)
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 8
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Mbangala umekuwa ukitengewa bajeti takribani kwa miaka mitatu sasa. Ni lini mradi huu utaanza kujengwa? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na labda nikiri kwamba nimeshafanya ziara kwenye Jimbo lake na tulikuwepo wote, huu ni mradi wa kimkakati katika eneo la Mheshimiwa Mchungahela.
Mheshimiwa Spika, Serikali tukipata fedha mradi huu utaanza mara moja ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 9
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia swali la nyongeza. Je, kuna mkakati gani wa kupunguza tatizo la maji katika Kata ya Mikese na hasa Tarafa ya Mtego wa Simba?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali kwanza kabisa ni kuendelea kubainisha vyanzo vya maji ambavyo vitatuongezea maji katika mtandao wetu, lakini vile vile ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kulinda vyanzo vya maji pamoja na kujenga mtandao ili uendelee kuwafikia wananchi.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutatuma timu yetu ikafanye utafiti ili tujiridhishe fedha kiasi gani zinahitajika, ili tufahamu kwamba kama tutahitaji kujenga mradi mpya tujenge mradi mpya kama itahitaji kufanya extension ya mradi uliopo basi tutafanya hivyo ili wananchi wa kata hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 10
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Maji yanayotoka katika Mji wa Kasuru hayafai kwa matumizi ya binadamu, ni machafu sana. Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo hilo la maji katika Mji wa Kasuru?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Kasuru, kwanza kabisa tuna mradi wa zamani ambao ulikuwepo. kwa bahati nzuri nilifanya ziara Mkoa wa Kigoma na hususani eneo la Kasuru; lakini pia tuna Mradi wa Miji 28 unaoendelea kutekelezwa pale, ambapo zaidi ya kata 19 zitapitiwa na mradi ule. Vilevile katika mradi wa zamani ambao ulikuwa unatumia maji kutoka kwenye kile chanzo kingine hatukuwa na chujuo ambalo ndiyo ilikuwa changamoto ya watu kupata maji ambayo hayakuwa safi.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitoa fedha kwa ajili ya kuanza kujenga chujio ili liweze kuyachuja maji na kuhakikisha kwamba tunapata maji safi, lakini pia tunayatibu ili tupate maji salama na pia tuwe na maji ya uhakika ambayo yatapatikana muda wote. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba chujio hilo litakapokamilika wananchi wa Kasulu watapata huduma ya maji ambayo yapo safi. Ahsante sana.
Name
Rehema Juma Migilla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuondoa tatizo la upungufu wa maji katika Mji Mdogo wa Karatu?
Supplementary Question 11
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi. Ninapenda kuuliza swali dogo la nyongeza. Bwawa la Ichemba lilitengewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi lakini fedha zile zilirudishwa makao makuu hatujui sababu hatujui sababu za kurudishwa. Je, ni lini fedha zile zitarudishwa ili mradi uanze kufanya kazi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kwa heshima na unyeyekevu na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri nipokee hii changamoto niende nikaone changamoto iliyojitokeza mpaka fedha zikarudishwa Wizarani wakati fedha hizi tunatakiwa kuzipeleka kule kwa ajili ya kwenda kutatua changamoto ya ujenzi wa miradi ya maji. Ninaomba nilipokee kwa ajili ya utekelezaji. Ahsante sana.