Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 135 2025-02-06

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka askari wa kutosha wa Jeshi la Uhifadhi Tunduru Kaskazini ili kumaliza athari zinazosababishwa na wanyama pori?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Wizara imepewa kibali cha kuajiri jumla ya askari 578 kupitia taasisi zake za uhifadhi. Askari hawa pamoja na majukumu mengine watatumika katika kushughulikia changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kwenye maeneo ya wananchi ikiwemo Tunduru Kaskazini.

Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua changamoto ya uchache wa askari katika Wilaya ya Tunduru kwani kwa sasa jumla ya Askari wa Jeshi la Uhifadhi 18 na askari wahifadhi wa vijiji 60 wapo katika Wilaya ya Tunduru. Katika juhudi za kupambana na changamoto hiyo ya uchache wa askari, Serikali ina mpango wa kuongeza askari wa Jeshi la Uhifadhi kutoka askari waliopo sasa 18 hadi kufikia Askari wa Jeshi la Uhifadhi 25 na Askari Wahifadhi wa Vijiji kutoka 60 hadi 80.

Mheshimiwa Spika, sambamba na askari hao, Serikali imepanga kuongeza vitendea kazi kwa ajili ya taasisi za Jeshi la Uhifadhi Kanda ya Kusini ikiwemo magari tisa, pikipiki 10 na ndege nyuki tano kwa ajili ya kuwawezesha kuongeza ufanisi wa kukabiliana na wanyamapori wakali katika Wilaya ya Tunduru na eneo lote la Kusini.