Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka askari wa kutosha wa Jeshi la Uhifadhi Tunduru Kaskazini ili kumaliza athari zinazosababishwa na wanyama pori?
Supplementary Question 1
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri yenye kuleta tija; lakini pamoja na majibu hayo mazuri naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; naishukuru na kuipongeza Serikali kwa kutupatia ndege nyuki moja ambayo inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana. Kwa kuwa tuna uhitaji mkubwa sana wa ndege nyuki, ndege nyuki ile inazidiwa. Je, ni lini hasa Serikali itatupatia ndege nyuki hizo tano ili zije kutatua kabisa changamoto?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Wilaya ya Tunduru ina hekta za mraba 18,778 na tunayo magari mawili ya askari wa wanyamapori. Kati ya magari mawili hayo moja ndilo linalofanya kazi vizuri lakini moja lina changamoto, halifanyi kazi. Ninataka kufahamu. Je, ni lini hasa magari hayo tisa yaliyozungumzwa yataletwa Wilayani Tunduru ili kuweza kutatua changamoto hiyo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba eneo la Mheshimiwa Mbunge ni maeneo ambayo yana changamoto kubwa ya wanyama wakali na waharibifu. Kwa kulitambua hili tayari Serikali kupitia wadau wa maendeleo na sisi wenyewe tumekwishanunua hizi ndege nyuki tano.
Mheshimiwa Spika, kinachofanyika sasa ni kuendesha mafunzo kwa askari wa vijiji 20 watakaotumika kuendesha ndege nyuki hizi. Mafunzo haya yanaendelea kwenye Chuo chetu cha Mafunzo ya Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga. Tunategemea mafunzo haya yatakwisha kwenye tarehe 15 hii mwezi Februari. Baada ya kukamilika mafunzo haya tutaelekeza nguvu kwenye eneo hili.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili la vifaa; mpango wetu kupitia taasisi zetu za uhifadhi ni kwamba tutaongeza magari tisa. Matarajio yetu ni kwamba ikifika mwishoni mwa mwezi Februari au mwanzoni mwa mwezi wa tatu magari haya yatakuwa yamekwishapatikana kulingana na zoezi la manunuzi na mara baada ya kupatikana tutayaelekeza kwenye maeneo haya.
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka askari wa kutosha wa Jeshi la Uhifadhi Tunduru Kaskazini ili kumaliza athari zinazosababishwa na wanyama pori?
Supplementary Question 2
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Katika Wilaya ya Ngara Kata ya Kasuru tembo wamevamia mashamba ya wananchi, wamekula mahindi, wamekula maharage mapaka migomba. Ningependa kujua, je, Serikali inatusaidiaje kuhusiana na kupeleka askari wa wanyamapori katika eneo hilo ili kutatua changamoto hiyo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kweli tunazo taarifa kwamba tembo wametoka kwenye Pori la Kimisi kwenda kwenye eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelisema.
Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu jana alipopata taarifa hii mara moja alitupa taarifa na sisi tulipowasiliana na askari wa uhifadhi kwenye eneo lile walisema ni kweli. Kuna timu ya utangulizi ya kundi la askari ilitumwa, lakini ilionekana kwamba kadhia iliyopo ni kubwa, kwa hiyo tumetoa maelekezo kwamba askari waongezwe zaidi ili kwenda kushughulikia tatizo hili. Tunalishughulikia, ninaomba Mheshimiwa Mbunge na wananchi wawe na subira wakati jambo hili linashughulikiwa.
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka askari wa kutosha wa Jeshi la Uhifadhi Tunduru Kaskazini ili kumaliza athari zinazosababishwa na wanyama pori?
Supplementary Question 3
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tarafa ya Mang’ula na Kidatu bado zinasumbuliwa na tembo. Je, ni lini Wizara itatuongezea askari wa uhifadhi pamoja na vifaa ili kudhibiti hali hiyo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwenye eneo hili kuna changamoto kubwa ya tembo na Serikali imefanya kazi kubwa. Eneo hili linalounganisha Hifadhi ya Udzungwa na Hifadhi ya Nyerere kuna ushoroba pale ambao ulikuwa umevamiwa. Serikali imefanya kazi kubwa sana ya kuongoa ushoroba ule kwa kujenga daraja la chini linalowezesha wanyama kupita. Hatua inayofuata sasa ni kuongeza askari katika eneo lile ili kuweza kukabiliana na changamoto hii ya wanyama wakali na waharibifu.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge amekuwa akija mara kwa mara. Kama nilivyomweleza tulipokutana, kwamba tayari tumepata kibali cha askari 575. Ni imani yangu ni kwamba baada ya kupatikana kwa kibali hiki na askari hawa kuajiriwa tutaelekeza nguvu ya kuongeza askari kwenye eneo lake. Ninaomba awe na subira.
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka askari wa kutosha wa Jeshi la Uhifadhi Tunduru Kaskazini ili kumaliza athari zinazosababishwa na wanyama pori?
Supplementary Question 4
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, utumiaji wa ndegenyuki kwa ajili kukabiliana na wanyama haribifu, hasa tembo, imeleta ufanisi mkubwa katika Wilaya ya Tunduru. Kwa kuwa Wilaya ya Tunduru inapakana na Wilaya yangu ya Nanyumbu. Je, Serikali haioni haja na sisi Wilaya ya Nanyumbu tukapatiwa ndegenyuki moja ili kukabiliana na wanyama hawa waharibifu?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kwamba tayari tumekwishanunua ndegenyuki tano kwa ajili ya kuhudumia ukanda huu wa kusini. Mheshimiwa Mbunge awe na amani, ombi lake litakuwa ni sehemu ya maeneo ambayo yatapatiwa ndegenyuki hizi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved