Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 47 2025-01-30

Name

Rose Cyprian Tweve

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaweka adhabu kubwa zaidi kwa wanaokutwa na hatia ya unyanyasaji?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, makosa mengi ya unyanyasaji yamebainishwa katika Sehemu ya 15 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, ambapo kuna makosa ya kubaka, kulawiti, kuzini na maalimu, shambulio la aibu, kunajisi punguani na kadhalika ambayo yana adhabu tofauti kulingana na aina na ukubwa wa kosa. Adhabu ya juu kwa makosa ya aina hii ni kifungo cha maisha jela na adhabu ya chini kabisa katika makosa haya ni kifungo cha miaka mitano kwa kosa la shambulio la aibu.

Mheshimiwa Spika, adhabu hizi zimewekwa kwa kuzingatia uzito wa kosa lililotendwa, hivyo Serikali bado inaamini adhabu hizo zinajitosheleza kuwa fundisho kwa wakosaji wa makosa haya.