Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rose Cyprian Tweve
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: - Je, lini Serikali itaweka adhabu kubwa zaidi kwa wanaokutwa na hatia ya unyanyasaji?
Supplementary Question 1
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana nami, pamoja na kuwa na hizo adhabu ambazo zimeainishwa na jitihada kubwa ambazo zimefanywa, bado changamoto ya unyanyasaji hasa kwa watoto ni kubwa. Hii siyo mara ya kwanza kuuliza swali hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge tukaonesha upungufu ambao upo katika sheria mbalimbali na Serikali ikafanya commitment kuwa itafanya utafiti na kutuletea baadhi ya sheria ambazo wanaona zina upungufu ili tuweze kuweka adhabu kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, moja ya upungufu ambao tulionyesha ni kuwa mtoto wa miaka 18 anaweza kubaka mpaka mara tatu ndiyo apate hiyo adhabu kubwa. Adhabu ya kwanza, anapata tu viboko, akibaka mara ya pili, ni miezi 12 na viboko. Sasa nilitaka kujua, ule utafiti Serikali mliosema mtaufanya umefikia wapi? Nashukuru. (Makofi)
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa swali moja la nyongeza linalohusu tumefikia wapi katika tafiti?
Mheshimiwa Spika, suala la tafiti ni jambo pana kidogo na linahitaji muda wa kutosha. Tunaendelea na utafiti kupitia taasisi yetu ya Law Reforms ambao wanaendelea kupitia mambo mbalimbali ikiwepo maoni na mapendekezo mbalimbali ambayo yametolewa na Waheshimiwa Wabunge. Kwa sasa, muda wowote wanaweza wakakamilisha tafiti zao na watatupa majibu ambayo tutayafikisha kwako, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved