Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Water and Irrigation Wizara ya Maji 48 2025-01-30

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Isale unaolenga kunufaisha vijiji sita vya Isale, Msilihofu, Ntuchi, Ifundwa, Kitosi na Nkata. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji (intake), ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 70.22, ujenzi wa matanki sita yenye jumla ya ujazo wa lita 420,000 na ujenzi wa vituo 75 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 78% na umeanza kutoa huduma ya maji kwenye vijiji viwili vya Nkata na Kitosi. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na kunufaisha wananchi 20,113 wa vijiji hivyo. (Makofi)