Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Licha ya majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Miradi mingi ya maji inachukua muda mrefu kukamilika kwa sababu wakandarasi wanachukua muda mrefu kulipwa. Je, kuna mkakati gani wa kulipa hawa wakandarasi kwa wakati ili miradi ikamilike kwa wakati? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini mradi wa maji Bwawa la Mindu, Manispaa ya Morogoro utakamilika ili wananchi wa Manispaa ya Morogoro wapate maji ya kutosha na ya uhakika? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Serikali ina mkakati wa kuhakikisha kwamba wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya maji wanalipwa kwa wakati ikiambatana na wao kuwasilisha hati za madai ambazo zinaendana na kazi ambayo wanakuwa wameifanya. Kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, tunaendelea kuangalia namna bora zaidi ya kuharakisha malipo kwa wakandarasi hao.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bwawa la Mindu, tupo ndani ya mkataba na mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa mradi huo. Lengo ni kwamba mradi ukamilike kwa wakati na wananchi wa Morogoro wapate huduma ya maji safi na salama, ahsante. (Makofi)
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 2
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nataka kujua, ni lini Serikali itapeleka fedha ili kukamilisha mradi wa maji Itumba – Isongole, kwa sababu mradi huu ni wa muda mrefu na wananchi wanakosa maji, kwani mabomba waliyoyaweka yanaendelea kupasuka kwa sababu ya kupigwa na jua?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba miradi yote ya maji inapelekewa fedha. Vilevile tunapeleka fedha kulingana na hati ambazo wakandarasi wameleta. Tumekuwa tukikutana na baadhi ya changamoto, wakandarasi hawatekelezi kwa wakati, lakini tumekuwa tukichukua hatua kukatisha mikataba na wakandarasi wazembe.
Mheshimiwa Spika, lengo ni kwamba tuweze kuleta mkandarasi ambaye ataendana na speed ambayo sisi tunahitaji ya kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa eneo la Songwe tutatoa kipaumbele kuhakikisha kwamba mkandarasi huyo anatekeleza mradi huo na ukamilike kwa wakati, ahsante sana. (Makofi)
Name
Shabani Hamisi Taletale
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 3
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa Kata ya Mkambarani?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mradi ambao Mheshimiwa Hamisi Taletale ameutaja ni kwamba tulikuwa na changamoto kidogo, mkandarasi akawa hayupo site na baadaye Serikali tumekaa mezani, tunaendelea na maongezi naye ili kuhakikisha kwamba anarejea site ili aweze kuendelea na mradi huo kwa sababu unalenga kuhudumia watu wengi ambao wana changamoto ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, jambo lake kwa sababu tayari ameshafika ofisini kwetu, tumeshaongea na liko katika hatua nzuri. Tunaamini kwamba litakamilika hivi karibuni. Ahsante sana.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 4
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ni lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Wilaya ya Tarime na Rorya utakamilika ili kuweza kuondoa changamoto za maji kwa wananchi wale? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni ndoto ya Waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mara akiwemo Mheshimiwa Esther Matiko na hakika ameendelea kulisemea sana mara kwa mara.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie kwamba miradi ambayo ipo katika mpango wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali, tutahakikisha inakamilika kwa wakati kulingana na muda wa mkataba ambao tumesaini na wakandarasi, ahsante sana.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 5
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini mradi wa Ziwa Victoria utakamilika katika Mkoa wa Simiyu? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, mradi wa kutoka Ziwa Victoria – Nyashimo – Bariadi – Itilima ambao una phase mbili, phase ya kwanza ikiwa inahusisha Wilaya tatu na phase ya pili ikiwa inahusisha Maswa pamoja na Meatu. Kwa phase ya kwanza umeshaanza na uko zaidi ya 25% lakini kwa awamu ya pili ambayo inahusisha Maswa pamoja na Meatu tayari tumeshatangaza tenda ya kumpata mkandarasi ambaye ataenda kutekeleza mradi huo.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi huu upo katika hatua nzuri na tunaenda vizuri kulingana na makubaliano yaliyoko kwenye mkataba. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 6
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, swali la msingi limezungumza kuhusu Kata ya Isale ipo Jimbo la Nkansi Kaskazini. Mradi huu una zaidi ya miaka 12. Naomba kufahamu, nini kimesababisha mpaka sasa ndiyo mradi umefikia 78%, na ni lini utakamilika? Nakushukuru.
SPIKA: Sasa hapo umeuliza maswali mawili, chagua moja. Chagua moja kati ya hayo mawili.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, ni lini mradi huu ambao umechukua zaidi ya miaka 12 utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, natambua na Serikali inatambua changamoto ya mradi huu ambapo Mkandarasi Fally Enterprises mwaka 2017 alipatiwa mkataba wa kutekeleza, lakini kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake, alisuasua sana na Serikali tukachukua hatua ya kusitisha mkataba. Baada ya kusitisha mkataba huo tukapata kampuni nyingine inaitwa Vibe International ambayo tuliingia mkataba na Serikali mwaka 2022. Sasa hivi, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi, mradi huu unatarajiwa kukamilika Juni, 2025. Ahsante sana.
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza Mradi wa Maji Isale Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 7
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, Mji wa Kinesi wenye population zaidi ya watu 10,000 hauna maji kwa zaidi ya miezi mitatu kwa sababu ya uharibifu wa pampu. Nini kauli ya Serikali?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan haiwezi kuvumilia pale ambapo tuna uwezo wa kuchukua hatua na Watendaji wasichukue hatua. Napenda kutumia fursa hii kumwelekeza RM Mkoa wa Mara kwenda katika eneo ambalo Mheshimiwa Jafari Chege amelizungumzia ili wakaangalie tatizo lilivyo na waweze kuchukua hatua ya kutatua changamoto hiyo na wananchi wa eneo hilo waanze kupata huduma ya maji safi na salama. Ahsante.