Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 3 Water and Irrigation Wizara ya Maji 49 2025-01-30

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti ambayo ni ahadi ya Waziri wa Maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti Wilayani Arumeru. Kazi zinazofanyika katika mradi huo ni ujenzi wa tanki la kukusanyia maji (sump well) lenye ujazo wa lita 50,000, ununuzi na ufungaji wa pampu mbili zenye uwezo wa kuzalisha maji lita 1,560,000 kwa siku, ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa kilometa 67, pamoja na ujenzi wa vituo 70 vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi umefikia wastani wa 80% na umeanza kutoa huduma katika maeneo ya Olmringaringa na Kimnyaki kupitia vituo 13 vilivyojengwa. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na utanufaisha wananchi wapatao 57,541 waishio maeneo hayo. Ahsante.