Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti ambayo ni ahadi ya Waziri wa Maji?

Supplementary Question 1

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na jitihada zilizofanyika kwa kiwango hicho. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa kuwa wananchi hawa wa Vitongoji hivyo vya Siwandeti, Kiranyi, Tarakwa na Kimnyaki wanateseka sana kwa ukosefu wa maji kutokana na wingi wao: -

(a) Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuharakisha mradi huu ili uweze kukamilika haraka na mapema zaidi?

(b) Je, pia ni lini Serikali itasambazia wananchi wa Kata ya Mlangarini, Kijiji cha Kiserian, Vitongoji vya Olmaroroi na Muungano ambapo bomba kubwa limepita katikati yao ili waweze kupata maji ili waweze kuondokana na adha ya ukosefu wa maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi, mradi huu umefikia 80% na tunatarajia utakamilika mwezi Juni.

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida, mradi huu unaweza ukakamilika ndani ya miezi mitatu, lakini kuna kipengele cha testing and commissioning ambacho kitahitaji kama miezi mitatu tena. Kwa hiyo, tunaamini kwamba, mpaka ifikapo Juni, wananchi wa maeneo hayo ambapo Mheshimiwa Mbunge amekuwa akiwapambania sana, basi watapata huduma hiyo ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, kwa kipengele cha pili, katika Vitongoji vya Muungano na vingine hivyo ambavyo vimepitiwa na bomba kuu, kwa sera yetu ni kwamba, vijiji na vitongoji vinavyopitiwa na bomba kuu kilometa 12.5 kulia na kushoto ni lazima wapate huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anatambua kwamba juzi alikuwepo katika vitongoji vile na sisi kama Wizara tulipokea changamoto ya wananchi waliyoiwasilisha kwa Mheshimiwa Mbunge. Sisi tuliichukua na kutolea maelekezo na kuwaelekeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha ili wahakikishe kwamba wanaharakisha usambazaji wa maji kwa wananchi wa vitongoji hivyo ili waweze kunufaika na huduma ya maji safi na salama. Ahsante.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti ambayo ni ahadi ya Waziri wa Maji?

Supplementary Question 2

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi na usambazaji wa maji katika Mji wa Mererani unaotekelezwa na Mamlaka ya Mji Arusha?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi ya maji ni maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan; na miongozo ya Mheshimiwa Waziri wetu ni kuhakikisha kwamba miradi hii inapokuwa inapata fedha bila kuwa na mkwamo wowote, basi ikamilike kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, natumia fursa hii kuwaelekeza Mamlaka ya Maji Arusha kuhakikisha kwamba Mradi wa Maji Mererani ukasimamiwe kwa ukamilifu, ukamilike kwa wakati na uwe una ubora unaotakiwa na wananchi wapate maji safi na salama yenye gharama inayokubalika. Ahsante sana.

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti ambayo ni ahadi ya Waziri wa Maji?

Supplementary Question 3

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mtwara Mjini ni jimbo ambalo tunakunywa maji ambayo ni ya visima na visima hivyo vimechimbwa miaka takribani 60 iliyopita. Kwa sasa tuna hali ngumu, baada ya muda, inawezekana maji yakapotea. Je, ni lini Serikali itatuwezesha fedha za kuchimba visima vingine virefu ili maji yaendelee kupatikana kwenye Jimbo la Mtwara Mjini? Nakushukuru.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, tunapata maji kwa njia mbili, surface water na underground water. Changamoto ya underground water ni kwamba hata kama tutaendelea kuchimba visima vingi, bado changamoto ya visima vingine kuendelea kukauka ni kubwa. Ndiyo maana tunachimba visima kwa ajili ya dharura na kutatua changamoto kwa muda mfupi na muda wa kati huku tukiwa tunaendelea kusanifu miradi mikubwa ambayo itakuwa suluhisho ambalo litasaidia wananchi kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, katika Mji wa Mtwara na Mtwara yenyewe, tunaendelea na miradi ile mikubwa ambayo ninaamini kwamba hiyo ndiyo itakuwa solution kubwa kwa ajili ya wananchi wa Mtwara kupata huduma ya maji safi na salama na ikiwa endelevu. Ahsante sana.

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Kata ya Kimnyaki, Tarakwa, Kiranyi na Siwandeti ambayo ni ahadi ya Waziri wa Maji?

Supplementary Question 4

MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itaanzisha mradi mkubwa wa maji kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere kuelekea Mkoa wa Lindi na Mtwara likawa suluhisho la kudumu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, katika vyanzo ambavyo ni vya uhakika vya maji ni Bwawa la Mwalimu Nyerere. Bwawa hilo litakuwa na uwezo wa uzalishaji wa maji wa lita nyingi zaidi kuliko bwawa lolote. Sisi Wizara ya Maji tayari tumeshaelekeza wataalamu wetu wafanye tathmini na kuangalia namna gani tutaweza kuingia kwenye kutafuta mtaalamu mshauri ili tuweze kutangaza tenda na kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Ahsante.