Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 3 | Finance | Wizara ya Fedha | 50 | 2025-01-30 |
Name
Ndaisaba George Ruhoro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngara
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga kufanya kazi saa 24?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Forodha cha Kabanga ni kituo cha pamoja cha kutoa huduma za forodha baina ya Tanzania na Burundi. Kituo hicho kina miundombinu wezeshi kama vile taa za ulinzi, vyombo vya ulinzi na usalama, na maeneo ya kukagulia bidhaa, wasafiri na wafanyakazi, hivyo kuwa na uwezo wa kufanya kazi saa 24 kwa upande wa Tanzania. Hata hivyo, ili kituo hicho kiweze kutoa huduma saa 24, upande wa Kobero nchini Burundi unapaswa pia kuwa tayari kutoa huduma hiyo saa 24.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa Kituo cha OSBP Kobero kwa upande wa Burundi kinatoa huduma kwa masaa 12 tu. Aidha, jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kuwezesha mazingira ya kituo cha OSBP Kobero kufanya kazi kwa saa 24, hususan ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Murusagamba ni kituo kidogo cha uzuiaji cha forodha (preventive office), vituo hivi hufanya kazi ya kuzuia magendo kwenye maeneo ambayo mwenendo wa bidhaa na watu ni mdogo. Kutokana na udogo wa mwenendo wa bidhaa na watu katika Kituo cha Murusagamba, uwezekano wa kutoa huduma kwa saa 24 haupo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved