Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga kufanya kazi saa 24?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maelezo ya Serikali kuhusu Kituo cha Murusagamba. Pamoja na jitihada hizo za Serikali, je, Serikali ina mpango gani wa kuweka cargo scanner upande wa Mutukula ili mizigo iweze kupita kwa kasi kwenda Afrika ya Kaskazini?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Mwijage kwa ufuatiliaji wa karibu wa suala hili. Ninayo furaha kumwambia Mheshimiwa Mwijage kwamba tayari mkandarasi yuko kwa ajili ya site kufunga mdaki huo mkubwa ahsante.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga kufanya kazi saa 24?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza ushuru wa forodha kwa magari yanayoingizwa kwa ajili ya huduma za afya na elimu?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka miongozo, taratibu, kanuni na sheria mbalimbali ambazo ninaamini Mheshimiwa Mbunge naye anazijua kwa kusamehe kodi kwa magari hayo ya afya na mengineyo ambayo uthibitisho umepatikana kutokana na Wizara ambazo zinastahiki.
Name
Mohammed Said Issa
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Konde
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga kufanya kazi saa 24?
Supplementary Question 3
MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Forodha cha Malindi – Zanzibar kinahudumia zaidi ya kontena 2000 kwa mwezi lakini kinafanya kazi kwa saa 12 tu, je, ni lini kitafanya kazi kwa masaa 24 ili kuongeza ufanisi? Nakushukuru.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyogeza la Mheshimiwa Mohamed, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwa sasa kituo chetu kile kinafanya kazi saa 12 tu, lakini tayari tumeshakaa na wenzetu upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Zanzibar. Mazungumzo yanaendelea, basi tukifikia mwafaka wa jambo hilo, tutatoa huduma kwa saa 24.
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha Vituo vya Forodha vya Murusagamba na Kabanga kufanya kazi saa 24?
Supplementary Question 4
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Horohoro kule Tanga hakina scanner, na hii inasababisha usumbufu mkubwa. Ni lini kitafungwa scanner, jambo ambalo ni muhimu kwa mapato ya nchi yetu?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge. Ni kweli anachokisema, na tayari Serikali kupitia TRA tumetenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa midaki mbalimbali. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba midaki itakayokuja ndani ya mwaka huu wa fedha, basi tutaingalia sehemu ya Horohoro na yenyewe, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved