Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2000-2005 Session 12 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 138 2025-02-07

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka Gari la Mkuu wa Wilaya ya Tarime?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali ilitenga na kuidhinisha shilingi Milioni 504.7 kwa ajili ya ununuzi wa magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser Prado kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya ya Tarime na Musoma.

Mheshimiwa Spika, taratibu za malipo kwa ajili ya ununuzi wa magari hayo zimefanyika Januari, 2025 kupitia kwa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) na hatua za manunuzi zinaendelea.
Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kuyapata magari hayo likiwemo gari la Mkuu wa Wilaya ya Tarime ndani ya mwaka huu wa fedha, ahsante.