Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Gari la Mkuu wa Wilaya ya Tarime?
Supplementary Question 1
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, hata hivyo, nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Tarime Vijijini ina Idara Tisa. Idara zenye magari ni mbili tu: Idara ya Miundombinu, Kilimo na Mifugo, Utawala, Maendeleo ya Jamii; lakini Mkaguzi wa Ndani, Sheria na TEHAMA hawana magari, na vitengo vyote havina magari. Je, ni nini utaratibu wa Serikali kuwawezesha watumishi hawa wa Serikali katika Halmashauri ya Tarime pia na nchi nzima ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na wanapotakiwa kufika kwa wananchi wafike kwa wakati, watatue changamoto za wananchi wetu? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kununua magari kwa ajili ya usimamizi, usambazaji na ufuatiliaji katika halmashauri zetu kote nchini. Katika mwaka wa fedha uliopita Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipeleka magari ya usimamizi wa huduma za afya katika Halmashauri zote 184, ikiwemo Halmashari ya Wilaya ya Tarime na magari ya Idara na Vitengo vingine yameendelea kupelekwa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwanza, magari yanayokuwa kwenye idara moja au kitengo kimoja pia yanaweza kutumiwa na idara nyingine. Tunafanya kazi kwa ushirikiano ndani ya Halmashauri. Vile vitengo ambavyo havina magari, Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa awamu kwa ajili ya kupeleka magari ili usimamizi uwe na ufanisi mkubwa zaidi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved