Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 139 2025-02-07

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, lini Serikali itatenga dirisha maalum la mikopo ya Wanaume waliovuka umri wa Kijana?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, mikopo ya 10% inatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 Kifungu cha 37A ya mwaka 2018 na Kanuni za usimamizi na utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2024.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria hii, mikopo ya 10% inatolewa kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo isiyo na riba. Makundi haya yana fursa ndogo ya kupata mikopo katika taasisi nyingine za fedha kwa kuwa yanakosa dhamana na uwezo mdogo wa kumudu riba.

Mheshimiwa Spika, aidha, umri wa ukomo katika mikopo kwa vijana umeongezwa kutoka miaka 35 hadi 45.

Mheshimiwa Spika, makundi mengine ambayo siyo walengwa wa mikopo hii wanashauriwa kupata mikopo kupitia taasisi nyingine za fedha, biashara na programu za kijasiriamali zinazohusisha makundi yote, ahsante.