Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga dirisha maalum la mikopo ya Wanaume waliovuka umri wa Kijana?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, kwa kweli kusema mikopo imeongezeka kutoka miaka 35 mpaka miaka 45 hilo nilikuwa silijui. Sasa kwa sababu imeongezeka, na huko vijijini wanasema umri wa vijana ni miaka 18 mpaka 30, je, ni lini sasa Serikali itatoa mwongozo kwa Halmashauri za Wilaya ili hawa watu wapate fursa ya kukopa, kwa sababu kuna gap kubwa kati ya watu 30 mpaka 35?

Mheshimiwa Spika, sasa tungependa kujua kama Serikali inaweza kuongeza hilo suala la kutoka miaka 30 hadi miaka 45. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali itoe mwongozo kwa Halmashauri za Wilaya ili suala hili liweze kutekelezeka kwa vijana, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa kanuni za mikopo ya 10% za mwaka 2024, miongozo tayari imeshatolewa na kupelekwa kwenye Halmashauri zote 184. Tangu mikopo imeanza kutolewa vijana wote wenye umri kati ya miaka 18 mpaka miaka 45 wanapewa mikopo.

Mheshimiwa Spika, natumia nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuendelea kuwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwamba umri wa vijana umeongezeka kutoka kikomo cha miaka 35 mpaka kikomo cha miaka 45 ili wanufaika waongezeke na kupata hiyo fursa ambayo ipo kwa ajili yao, ahsante. (Makofi)

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga dirisha maalum la mikopo ya Wanaume waliovuka umri wa Kijana?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, kundi la akina mama waliozaa watoto wenye ulemavu wamekuwa wakipata shida sana kuwalea, na kwa kuwa hawakopesheki kwa akina mama na wala hawakopesheki kwenye kundi la watu wenye ulemavu, je, ni lini Serikali itaona umuhimu kwa hawa akina mama waliozaa watoto wenye ulemavu, waweze kuwekewa kifungu maalum ili wakopesheke japo kwenye kikundi cha walemavu, kwa sababu wengi wao wanaume wamewakimbia kwa sababu ya kuzaa watoto wenye ulemavu? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, aakina mama ambao wanalea watoto wenye ulemavu, kwanza wanazo sifa ya kujiunga na vikundi vingine vya wanawake ili kupata ile mikopo ya 10%.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwanza tunawashauri hawa akina mama wajiunge na makundi mengine ya wanawake yaliyopo katika maeneo yao ili waweze kunufaika na mikopo ya 10%.

Mheshimiwa Spika, pili, tutaendelea kuona namna nzuri ya kuboresha mfumo na kuwapa zaidi kipaumbele wale ambao wanalea watoto au watu wenye ulemavu, ambapo walemavu wenyewe wasingeweza kufanya biashara, lakini walezi wanaweza kufanya biashara. Serikali imeendelea kuwapa kipaumbele katika mikopo ili waweze kutoa huduma hiyo ipasavyo, ahsante. (Makofi)

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga dirisha maalum la mikopo ya Wanaume waliovuka umri wa Kijana?

Supplementary Question 3

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa mwongozo uliotolewa sasa hivi, Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani hawaruhusiwi kushiriki katika zile Kamati za kutambua vile vikundi vinavyokopeshwa.

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini hawa viongozi wametolewa wakati ndio wanaowafahamu hawa wananchi? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, katika muundo wa sasa wa mikopo ya 10%, kuna Kamati za Watalaam ambazo zinahusika na mikopo hiyo ngazi ya Kata na ngazi ya Wilaya, lakini viongozi ambao ni wanasiasa katika maeneo hayo nao wanahusika kwa namna moja au nyingine, hawako kwenye zile Kamati moja kwa moja, lakini wanahusika kuhamasisha, wanahusika pia kufuatilia vikundi kama vimepata mikopo? Pia wanahusika kufuatilia urejeshaji wa mikopo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, siyo kwamba wametolewa, ni utaratibu ulioboreshwa lakini wanaendelea kuhusika kuhakikisha kwamba vikundi vile vinanufaika na mikopo lakini marejesho yanarejeshwa kwa kadri ya utaratibu, ahsante.