Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 140 2025-02-07

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha maboma ya nyumba za Walimu na Waganga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi – Mkalama?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ina jumla ya maboma 54 ya nyumba za watumishi wa Elimu na Afya ambayo yanahitaji ukamilishaji. Kati ya maboma hayo, maboma ya nyumba za watumishi wa afya ni nane na elimu ni 46.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri imeendelea kutenga fedha za kukamilisha maboma ya nyumba za watumishi kupitia mapato ya ndani ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024 jumla ya maboma sita ya nyumba za waganga katika zahanati za Endasiku, Mgimba na Kinankamba pamoja na nyumba za walimu katika shule za Ishenga, Kinyangiri na Mbigigi zimekamilishwa kwa gharama ya shilingi milioni 113.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 Halmashauri inatarajia kutenga shilingi milioni 100 ajili ya ukamilishaji wa nyumba mbili (three in one) za watumishi wa Afya.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya nyumba za watumishi katika Sekta ya Afya na Elimu kwa awamu.