Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha maboma ya nyumba za Walimu na Waganga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi – Mkalama?

Supplementary Question 1

MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali ambayo yanatia moyo, lakini ufanisi wake utakuwa mdogo, ukizingatia kwamba Halmashauri zetu hazifanani kwa mapato. Halmashauri yangu ya Mkalama ni Halmashauri mpya, mapato yake ni kidogo sana. Magofu haya ambayo wananchi wamejenga hizi nyumba kwa gharama zao za kilimo ni mengi. Je, Serikali haioni kwamba sasa majibu haya ya kusukumia Halmashauri, yanazidi kuchelewesha na zile nguvu za wananchi zinapotea?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sasa iweke bajeti maalum kwa ajili ya kumalizia magofu haya ili wananchi waweze kupata huduma stahiki?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Francis Isack Mtinga kwa swali lake zuri kabisa linalolenga kuhakikisha miundombinu mizuri na nyumba zinapatikana kwa ajili ya watumishi wetu katika kada ya afya na Elimu.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hoja yake ni ya msingi na ndiyo maana Serikali kupitia Wizara ya Fedha imetoa tamko kwamba, hivi karibuni tutapokea fedha kwa ajili ya kwenda kukamilisha baadhi ya maboma ambayo yameanzishwa kujengwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hizi fedha zitakazotoka Wizara ya Fedha zinalenga pia kugusa ukamilishaji wa miundombinu ya nyumba kwa ajili ya watumishi wetu kwenye kada ya afya na elimu. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge akae kwa mikono ya kupokea kwa maana Serikali italeta fedha kuongeza nguvu katika ujenzi wa hii miundombinu. (Makofi)

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha maboma ya nyumba za Walimu na Waganga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi – Mkalama?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imeahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha maboma, je, Mkoa wa Shinyanga pia utakuwa miongoni mwa mikoa hiyo itakayopata fedha?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mnzava kwa kupambania sana maslahi ya Mkoa wake wa Shinyanga. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inadhamiria kugusa siyo tu Mkoa wa Shinyanga bali mikoa yote ya Tanzania Bara kwa ajili ya kuhakikisha inakuja kuunga mkono jitihada za wananchi walioanzisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali iliyofikia katika ngazi ya maboma, kwa kuongeza nguvu ili kukamilisha maboma haya. (Makofi)

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha maboma ya nyumba za Walimu na Waganga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi – Mkalama?

Supplementary Question 3

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza nyumba za watumishi katika Hospitali ya Mji wa Nanyamba, ambapo kwa sasa kuna nyumba moja tu ya mtumishi? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Chikota kwa maana amekuwa akifanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha kwamba watumishi wanapata mazingira bora ya kufanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inatambua umuhimu wa watumishi kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na ndiyo maana Serikali imeanza kujenga nyumba za watumishi mbalimbali kwenye kada ya afya na elimu.


Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na jitihada hizo ili kutengeneza miundombinu itakayotosheleza watumishi wetu kufanya kazi na kuwa na mazingira mazuri ya kuishi na kufanya kazi katika mazingira bora zaidi.