Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 141 2025-02-07

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule Shikizi za Msingi zilizoanzishwa kwa nguvu za Wananchi – Kilolo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ina jumla vituo shikizi 18 vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi ambavyo ni Kichangani, Msombwe, Mlewela, Madizini, Igingilanyi, Mabondwa, Kware, Mapangali, Muungano, Lugolofu, Ilangamoto, Ubandusi, Barabarambili, Kidumka, Lulindi, Kitemela, Kisanzala na Masimike.


Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2024/2025, Serikali ilipeleka shilingi milioni 701 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya za mkondo mmoja katika vituo shikizi vya Kichangani na Msombwe. Ujenzi wa shule hizi upo hatua ya ukamilishaji.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika vituo shikizi vilivyoanzishwa kwa nguvu za wananchi kadri ya upatikanaji wa fedha.