Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule Shikizi za Msingi zilizoanzishwa kwa nguvu za Wananchi – Kilolo?
Supplementary Question 1
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, pia napenda kuishukuru Serikali kwa kuleta fedha za kujenga shule mbili, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Pamoja na shule shikizi, lakini ziko shule chakavu ambazo zimejengwa miaka mingi iliyopita kama Shule ya Msingi ya Idete, Shule ya Msingi Boma la Ng’ombe na Shule ya Msingi ya Ilole, hali zake ni mbaya sana. Je, Serikali ina mpango gani maalum wa kupeleka fedha ili shule zile ziweze kukarabatiwa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Shule shikizi mojawapo ya Lugolofu ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameitaja hapo, wananchi wameikamilisha, wamejenga madarasa mawili na vyoo, na watoto wanatembea kilomita 20 kufika shuleni. Je, Serikali iko tayari kupeleka walimu haraka ili wale watoto wadogo wa Darasa la Kwanza na la Pili, waanze kusoma pale na kuepuka usumbufu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Justin Nyamoga kwa kuendelea kupaza sauti kwa ajili ya wapiga kura wake wa Jimbo la Kilolo.
Mheshimiwa Spika, kwanza, Serikali imetenga fedha katika mwaka huu wa bajeti kwa ajili ya kufikia shule ambazo zimechakaa na miundombinu yake inahitaji kuboreshwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakaa mimi naye, nafahamu tayari alishaleta maombi, nitamweleza mchakato umefikia hatua gani?
Mheshimiwa Spika, pia Mheshimiwa Mbunge awaambie wapigakura wake wa Kilolo kwamba, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ipo tayari kwa ajili ya kuhakikisha inaboresha miundombinu hii muhimu katika shule hizi alizozitaja.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na uhitaji wa walimu naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari Serikali imetangaza ajira za walimu 10,015 na michakato ya usahili inaendelea. Walioomba wanafanyiwa usahili, watapatikana walimu watakaopangwa katika maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kwenda kuanza kufundisha. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutazingatia maombi aliyoyatoa ili kwenye hizo shule alizozitaja ziweze kupata walimu wa kuwafundisha wanafunzi wetu.
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule Shikizi za Msingi zilizoanzishwa kwa nguvu za Wananchi – Kilolo?
Supplementary Question 2
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Katika Jimbo la Moshi Vijijini, shule nyingi za msingi zilizojengwa kabla ya uhuru na mara baada ya uhuru zimechakaa sana. Naomba aniambie Serikali ina mpango gani wa kuzikarabati shule hizi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Prof. Ndakidemi kwa kazi nzuri ya kuwasemea wananchi wake na kuwapambania katika changamoto zao. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali katika mwaka huu wa fedha imetanga fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule chakavu.
Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuzifikia shule alizozitaja kwa ajili ya ukarabati ili wanafunzi wapate mazingira mazuri ya kusomea na walimu wapate mazingira mazuri ya kufundishia.
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule Shikizi za Msingi zilizoanzishwa kwa nguvu za Wananchi – Kilolo?
Supplementary Question 3
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali haioni haja ya kupeleka shule ya mkondo mmoja katika Kijiji cha Maweni ili kupunguza msongamano uliopo katika Shule ya Msingi Ng’oboko?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Leah Komanya kwa kupaza sauti yake kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wananchi katika jimbo lake wanapata elimu iliyo bora.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatekeleza mradi wa BOOST kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inapunguza msongamano katika shule za msingi ambazo zina wanafunzi waliozidi, na pia inapunguza umbali mrefu wa wanafunzi kufika shule.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge kwamba, Serikali inatambua uhitaji alioueleza na Serikali itaendelea kufika katika maeneo mbalimbali, ikiwemo katika jimbo lake kwa ajili ya kujenga shule hizi ili kupunguza msongamano.
Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule Shikizi za Msingi zilizoanzishwa kwa nguvu za Wananchi – Kilolo?
Supplementary Question 4
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya shule chakavu na shule kongwe, nami kwenye Jimbo langu kuna Shule ya Mchinga moja, hii ni shule ya tangu mwaka 1948 na imechakaa sana. Je, ipo miongoni mwa hizo fedha zilizotengwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Salma Kikwete, kwa kweli amekuwa akifuatilia sana ili kuhakikisha kwamba wapigakura wake wanapata elimu iliyo bora kwa kuwa amekuwa akiwasemea changamoto zao katika sekta hii muhimu ya elimu.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake, naomba nimhakikishie kwamba, ni dhamira ya Serikali kufikia shule chakavu na kuweza kuzikarabati ili ziwe na mazingira mazuri kwa ajili ya wanafunzi kusomea na walimu kufundishia.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mimi naye tutakaa, tutazungumza, tutapanga, lakini lengo ni kufikia shule hizi zinazotajwa ambazo ni chakavu ili ziweze kuboreshwa.