Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 142 2025-02-07

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. ALLY Y. MHATA aliuliza: -

Je, lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kutokana na hali halisi ilivyo nchini, kuna maeneo ya vijiji na vijiji miji ambapo maeneo ya vijiji yanaunganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000/= na maeneo yenye sura ya vijiji miji, yanaunganishwa kwa gharama ya shilingi 320,960/=. Kwa maeneo ya Kata ya Mangaka na Kilimahewa yenye sura ya vijiji miji yanaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 320,960/=. Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho kutokana na tathmini iliyofanyika, ahsante.