Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. ALLY Y. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY Y. MHATA: Mheshimiwa Spika, naomba nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, maeneo ya Kata hii ya Mangaka, yote yana sura ya vijiji na siyo vijiji mji.
Mheshimiwa Spika, je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kufuatana nami akaone hali halisi ya kata zangu ili maamuzi haya yafanyike kwa haraka iwezekanavyo kwa sababu wananchi wana hamu sana ya kupata umeme huu?
Mheshimiwa Spika, katika Wilaya yangu tunavyo vitongoji 105 ambavyo mpaka sasa hivi havijapata umeme. Je, Waziri anatoa kauli gani kuhusu vitongoji hivi 105, kwamba ni lini vitapata umeme?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mazuri ya Mheshimiwa Mbunge, na ninaomba niyajibu kwa Pamoja kwamba, kuhusu kuambatana na Mheshimiwa Mbunge, nitafurahi kwenda kwenye Jimbo la Nanyumbu na Mheshimiwa Mbunge ili tukayaangalie maeneo hayo. Kwa hiyo, nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya Bunge tutajipanga kwa ajili ya ziara hiyo.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na vitongoji 105 ambavyo havina umeme, kwa sasa Serikali ina miradi ambayo inaendelea ikiwemo vitongoji 15 vya Mbunge. Hata hivyo, kwa mradi ambao tutauanza mwaka huu wa fedha, tutaongea vitongoji vingine 38 ili kupunguza idadi hii ya vitongoji 105 ambayo imebakia.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni dhamira ya Serikali kuhakikisha tunaendelea kupeleka umeme kwenye vitongoji, na tumejipanga hivyo hata kwa mwaka huu wa fedha, ahsante.
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. ALLY Y. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani?
Supplementary Question 2
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, pamoja na kuishukuru Serikali kwa kutujengea kituo cha kupozea umeme Wilayani Urambo eneo la Uhuru, je, ni lini kituo cha kupozea umeme kitaanza kufanya kazi ili tuachane na tatizo la umeme tulilonalo?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Kituo hiki cha Kupooza Umeme cha Uhuru katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge tayari kimeshakamilika. Tunasubiri kukamilisha njia ya kusafirisha umeme ambayo ikikamilika ndipo kituo kitakapoanza kufanya kazi.
Mheshimiwa Spika, njia ya kusafirisha umeme tayari imefika asilimia nzuri. Wakandarasi kwa sasa wako site na wanafanya kazi hii kwa haraka sana ili kuhakikisha kwamba tunamaliza transmission line ili Kituo hiki cha Uhuru kianze kufanya kazi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved