Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Energy and Minerals Wizara ya Madini 143 2025-02-07

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapitia upya tozo zilizopo kwenye mnyororo wa uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu zinazowaelemea wachimbaji wadogo?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mkakati wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI) imefanya utafiti wa tozo 66 zinazotozwa na halmashauri katika shughuli za madini ikiwemo madini ya dhahabu. Tozo zilizobainika katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu ni pamoja na ushuru wa karasha, ada ya ukaguzi, VAT leaching, Mialo, ushuru wa kusafirisha miamba ya madini na visusi (mabaki ya miamba baada ya kuchenjuliwa).

Mheshimiwa Spika, katika kutatua changamoto hizi Wizara iliitisha kikao mwezi Agosti, 2024 Mkoani Singida ambacho kilishirikisha Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Wizara ya Fedha; Tume ya Madini; STAMICO; Halmashauri za Wilaya za Ikungi, Chunya, Kahama, Msalala, Meatu, Shinyanga, Mtama na Lindi; FEMATA; na TAWOMA. Rasimu ya mapendekezo ya maboresho tayari imeshaandaliwa na ipo katika hatua ya kufanyiwa mapitio na tathmini, ambapo matokeo ya tathmini hiyo yatatusaidia katika kupanga tozo rafiki kwa wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto za kikodi nchini, Mheshimiwa Rais ameunda Tume ya Maboresho ya Kodi ili ifanye tathmini ya mfumo wa kodi na kuleta mapendekezo ya namna ya kuboresha mfumo wa kodi. Ni imani yetu kuwa maboresho hayo yataangazia changamoto za kikodi zinazoikabili Sekta ya Madini.