Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: - Je, lini Serikali itapitia upya tozo zilizopo kwenye mnyororo wa uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu zinazowaelemea wachimbaji wadogo?

Supplementary Question 1

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali kuhusu tozo nyingi ambazo zinaambatana na mnyororo wa uchenjuaji wa dhahabu. Nina maswali mawili ya nyongeza: -

(a) Je, kwa vile wachimbaji wadogo wameendelea kulipa fedha hizi na mirabaha mingi kwenye uchenjuaji huu wa dhahabu, hamwoni sasa ni wakati mwafaka kwa Wizara ya Madini na TAMISEMI kukaa mapema ili hizi rasimu zinazosemwa zikamilike mapema ili wananchi (wachimbaji wadogo) waweze kupata unafuu?

(b) Je, Wizara ya Madini hawaoni kwamba ni muda mwafaka sasa wa kwenda kwenye mazingira ambayo kuna uchimbaji wa madini kuwasaidia watu wenye leseni na maduara ambao wanaendelea kubisha kila siku namna ya kugawana baada ya kupata mali?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwa swali kwanza tayari tumeshakaa na wenzetu wa TAMISEMI katika hatua ya awali, na hivi sasa jambo hili liko katika ngazi ya Makatibu Wakuu, baada ya hapo litawasilishwa ili tuweze kulitolea maamuzi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili linalohusu wenye leseni na wenye maduara, naomba nitumie fursa hii kuliarifu Bunge lako kwamba katika utatuzi wa changamoto hii tumetunga kanuni ambayo hivi sasa inapitiwa na wadau, ambayo inalenga kuhakikisha kwamba mwenye leseni na wenye maduara waingie makubaliano ili kuepusha migogoro.
Mheshimiwa Spika, sheria inataka kila anayepewa leseni achimbe yeye, asipangishe. Ukikubali kumwingiza mchimbaji mdogo kwenye leseni yako, ni lazima pia uingie naye makubaliano, ambapo ndiyo kanuni hiyo inasema ili tuondoe migogoro hiyo.