Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 144 2025-02-07

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama ya Wilaya Momba?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania, imeendelea kutekeleza mpango wa ujenzi na ukarabati wa Mahakama kwa kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyopo.

Mheshimiwa Spika, katika Mpango huo, ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Momba utatekelezwa kwa bajeti ya mwaka 2024/2025. Kwa sasa mradi huo upo hatua ya mwisho ya manunuzi ya kupata mkandarasi wa ujenzi. Hivyo, ujenzi unatarajiwa kuanza ndani ya mwezi Februari, 2025, ahsante.