Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama ya Wilaya Momba?
Supplementary Question 1
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza. Kwa kuwa mwezi huu ndiyo mwezi wa Pili sasa, na majibu yake yanaonesha kwamba ujenzi unaanza mwezi huu wa Pili, nataka kujua, je, wameshampata mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi huu?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Changamoto iliyopo Wilaya ya Momba ndiyo changamoto kubwa iliyopo Wilaya ya Ileje. Nataka kujua, Serikali mna mpango gani wa kujenga Mahakama nzuri na ya kisasa yenye hadhi ya wilaya ndani ya Wilaya ya Ileje?
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kuhusu kumhakikishia kama mkandarasi amepatikana, katika jibu la msingi nilisema wako katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi. Baada ya mkandarasi kupatikana, atakabidhiwa site na kwa mujibu wa Mahakama, mwezi huu ndiyo anatarajiwa kukabidhiwa site. Kwa hiyo, dada yangu Mheshimiwa Mbunge awe na uhakika kwamba litatekelezwa na vinginevyo mimi na yeye tutafuatilia ili kuona kwamba lengo hilo linafikiwa.
Mheshimiwa Spika, kuhusu uwepo wa ujenzi wa Mahakama ya aina hiyo Ileje, kama nilivyowahi kusema katika nyakati tofauti, Mahakama ina mpango mkakati wa miaka mitano mitano. Katika mpango mkakati huu wa awali, Ileje haikuwemo, lakini katika mkakati unaofuata tunatarajia Wilaya ya Ileje itaingia, ahsante.
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama ya Wilaya Momba?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. ANGELINE S. MABULA: Mheshimiwa Spika, Manispaa ya Ilemela ilitenga kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Sangabuye ili kuitoa katika lile eneo ambalo wana mwingiliano na Kituo cha Afya cha Sangabuye. Je, ni lini sasa Mahakama itakwenda kujenga katika kiwanja walichotengewa ili kuwapa uhuru Kituo cha afya kipanuliwe? Ahsante.
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge na Halmashauri ya Ilemela, moja, kwa kuhakikisha kwamba kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama kinapatikana. Nami nashukuru kwa taarifa hiyo nzuri.
Mheshimiwa Spika, tutakachokifanya kwa sasa niitake Mahakama, hasa Mtendaji Mkuu wa Mahakama na wataalamu wake wafuatilie kuona kiwanja hicho ili wakimiliki, kwanza kiwe chini ya Mahakama, na baada ya hapo, kiingizwe katika mpango wa ujenzi wa Mahakama inayohitajika pale Ilemela, nashukuru.
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mahakama ya Wilaya Momba?
Supplementary Question 3
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Je, ni lini Mahakama ya Wilaya ya Uyui itajengwa, kwa sababu mchakato peke yake umechukua miezi sita?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ni kweli katika mwaka huu wa fedha ambao tunaendelea nao, Mahakama za Wilaya 18 zinatarajiwa kujengwa ikiwemo Mahakama ya Wilaya ya Uyui.
Mheshimiwa Spika, ni matarajio yetu kwamba, Mahakama itakamilisha mchakato wa manunuzi; na kwa uhakika wamenihakikishia kuwa mwezi huu wa pili michakato itakuwa imekamilika ili kuwakabidhi wakandarasi site waweze kuijenga.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutafuatilia ili kuona kwamba ahadi ya kujenga Mahakama hiyo katika mwaka huu wa fedha inatekelezwa. Nashukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved