Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 145 2025-02-07

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA K.n.y. MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: -

Je, lini Serikali itafufua kiwanda cha kuchambua Pamba cha Nyakarilo, Buchosa?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bodi ya Pamba (TCB) mwaka 2020 ilifanya tathmini juu ya hali ya viwanda vya kuchambua pamba nchini. Tathmini hiyo imewezesha ukarabati wa baadhi ya viwanda hivyo. Viwanda vilivyokuwa vinahitaji ukarabati mkubwa ni pamoja na kiwanda cha kuchambua pamba cha Nyakarilo.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Benki ya Kilimo ilianzisha utaratibu wa dirisha maalum la kuvikopesha viwanda husika. Baadhi ya viwanda vilivyopata mikopo, kukamilisha ukarabati na kuanza kufanya kazi ni pamoja na Chato Cooperative Union, Mbogwe Cooperative Union, Kahama Cooperative Union na Sola. Kwa kutumia utaratibu huo, Serikali itahakikisha pia kiwanda cha Nyakarilo kinakarabatiwa ili kuongeza tija katika mnyororo mzima wa sekta ya pamba. Nakushukuru.